Mapambano makali Syria
13 Machi 2013MAPIGANO makali yametokea katika mji wa Homs nchini Syria katika ya waasi na vikosi vya utawala wa Rais Bashar Al-Assad na kukata mawasiliano ya barabara kuu inayounganisha mjini wa Damascus na uwanja wa ndege wa kimataiafa wa nchi hiyo.
Hayo yamesemwa na waangalizi wa shirika la kutetea haki za binadm nchini Syria wakiongea na shirika la habari la AFP. Mapigano hayo yanakujawiki moja baadaya utawala wa Rais Bashar Al-Assad kupeleka vikosi vyake ili kuwaondoa waasi wanaodhibiti mji wa Khaldiyeh karibu na mji mkuu wa Syria Damascus.
Kauli ya waangalizi katika mapigano
''Waasi na vikosi vya utawala wa Rais Bashar Al-Assad wamekuwa katika mapambano makali katika eneo la Baba Amr. Mapigano hayo yalizidi hasa katika barabara ya Brazil street, na vikosi vya utawala wa Syria vinadaiwa kutumia mabom na makombora ambayo yamehharibu vibaya mji wa Khaldiyeh''wamsema waangalizi wa haki za binadam.
Mapigano mapya pia yametokea katika jana katika eneo la Baba Amr, ambalo linatajwa kuwa ni eno muhimu na jirani ambalo limekuwa ngome ya utawala wa Rais Bashar al-Assad.
Mapigano katika mji wa Babr Amr
Mapema wiki hii waasi wa Syria walipanga kufanya mashambulizi makubwa ili kurudisha mji wa Babr Amr, ambao ulitokea mapigana ya silaha katika ya waasi na vikosi vya utawala wa Bashari Al -Assad
Mapigano hayo yanafanyika katika eneo hilo, kutokana na barabara hiyo kuwa muhimu na ndio njia kuu ya utawala wa Syria kuondoka nje ya nchi, na kuwa karibu zaidi na mji mkuu wa Syria Damascus.
Jana mapambano makubwa yameshuhudiwa Mashariki ya mji wa Jobar, ambapo waasi walikuwa wanadhibiti pembeni ya mji huo. Ni miaka miwili sasa Syria ikiwa katika machafuko ya kisisa ambayo yamepelekea zaidi ya watu 70,000 kufariki dunia na maelfu ya wengine kuishi wakiwa wakimbizi katika maeneo ya chi jirani ya Syria.
Mwandishi: Hashim Gulana/ AFP & Reuters
Mhariri: Moahammed Abdul-Rahman