1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAPAMBANO MAPYA GAZA:

23 Desemba 2003

GAZA: Si chini ya Wapalestina 8 na maafisa 2 wa Kiisraeli wameuawa katika Ukanda wa Gaza,baada kuzuka mapambano makali kabisa tangu miezi kadhaa hivi sasa.Wapalestina 6 walifariki na wengine 40 walijeruhiwa katika mashambulio yaliofanywa na vifaru vya Israel vilivyoivamia kambi ya wakimbizi ya Rafah.Hayo ni kwa mujibu wa duru za hospitali.Uvamizi huo ulitokea saa chache baada ya wanajeshi 2 wa Kiisraeli kuuliwa katika shambulio la ghafla katikati ya Gaza.Washambulizi 2 wa Kipalestina wakapigwa risasi na kuuliwa na vikosi vya Israel.Kwa mujibu wa duru za kijeshi za Israel,lengo la opresheni ya Rafah ni kuzisaka njia za chini kwa chini zinazotumiwa kusafirisha miripuko kwa njia ya magendo kutoka nchi jirani Misri.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW