1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapambano yaendelea Ufaransa

8 Novemba 2005

Paris:

Polisi wa Ufaransa wamesema leo kuwa magari 1,173 yamechomwa moto na watu 330 wamekamatwa jana usiku huku machafuko yakiingia siku ya 12 nchini humo. Maafisa wa polisi 12 wamejeruhiwa kidogo kutokana na mawe waliyotupiwa. Walikuwa lengo kubwa la mashambulio yanayofanywa na Vijana. Nyumba kadhaa nazo zimechomwa moto. Idadi ya magari yaliyochomwa moto na watu waliokamatwa ni ndogo ikilinganishwa na juzi usiku. Rais Jacque Chirac wa Ufaransa atakutana na Baraza lake la Mawaziri baadaye leo na kuwaruhusu Wakuu wa mikoa kutangaza hali ya hatari ikiwa ni lazima kufanya hivyo kwa lengo la kurudisha tena ufungamano wa Umma.