SiasaSudan
Mapambano yazidi kuzizima mjini Khartoum
10 Mei 2023Matangazo
Hayo yanajiri wakati wajumbe wa pande mbili zinazohasimiana Sudan wakiendelea na mazungumzo nchini Saudi Arabia ya kufikiwa makubaliano ya kusitishwa mapigano na kupelekwa msaada wa kitu. Wakaazi wameripoti mapigano makali ya ardhini katika viunga vya mji mkuu Khartoum, kati ya jeshi na wanamgambo wa kikosi cha Rapid Support (RSF). Mapambano ya silaha nzito pia yameshuhudiwa kaskazini mwa Omdurman na mashariki mwa Bahri, miji miwili ambayo Mto Nile ndio umeitenganisha na Khartoum. Tangu jana, jeshi limekuwa likiyalenga maeneo ya miji mitatu, likijaribu kuwaondoa wanamgambo wa RSF ambao wamechukua udhibiti wa maeneo makubwa ya makaazi na maeneo ya kimkakati tangu machafuko hayo yalipoanza Aprili 15.