1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAPATANO YA KYOTO YAANZA KAZI LEO

15 Februari 2005

Siku 90 baada ya Bunge la Urusi kuidhinisha mapatano ya Kyoto yanayolinda

kutochafuliwa kwa hali ya hewa, mapatano hayo yanaanza kufanya kazi leo hii,februari 16.Kwa kuanza kazi ile shabaha iliolengwa huko Kyoto,Japan 1997 –yaani kupunguza moshi na mivuke inayopaa hewani na hivyo kupunguza ujoto kumewekwa sasa chini ya msingi wa kisheria.

Siku ya leo Februari 16 inasherehekewa kote duniani-kuanzia Kanada-Ujerumani hadi Japan.Imnaadhimishwa leo kwa tafrija mbali mbali siku ya kuanza kutumika kwa mapatano ya Kyoto.Na sherehe hizo zinastahiki.Kwani, leo Februari 16,ni siku ya historia katika kutunza mazingira yetu na hali ya hewa duniani.Kwa upande mmoja dola kadha za kiviwanda zimejitwika hapa jukumu hadi ifikapo 2012 kupunguza moshi kutoka viwanda na vinu vyao unaopaa hewani kwa kima cha 5% kila mwaka kuliko ilivyokua 1990.

Kwa upande wapili, na haya ni mafanikio makubwa, mapatano haya yameingiza chombo cha uchumi wa soko katika kutunza hali ya hewa.

Mapatano yalioafikiwa juu ya biashara ya kupunguza moshi na mvuke duniani inafanya kuchafua mazingira kuwe na gharama yake ya kulipa.Kwa upande mwengine yanatoa uwezekano hata katika miradi katika nchi changa, kupunguza kuchafua mazingira kuletze nafuu za gharama.

Ni ushawishi gani nguzo hii ya kiuchumi inachangia kuzuwia kuchafua hali ya hewa kumebainishwa tayari na biashara ya kupunguza moshi barani Ulaya ambayo UU tayari mwanzoni mwa mwaka huu imeanza kufanya.

Lakini licha ya furaha yote iliopo kwa kuanza kazi kwa mapatano ya Kyoto na kumalizika kwa mvutano wa muda mrefu juu ya hatima ya mkataba huu,unasalia kwa hatua ya kwanza tu kuelekea njia ndefu ya kupunguza hasa uchafuzi wa hali ya hewa.

kimsingi kuzidi kwa ujoto katika sayari yetu ni jambo lisiloweza tena kuzuwilika,kwani kumeshaanza.Kwani,mnamo miaka 200 iliopita binadamu wamekuwa wakichafua mno mazingira kwa kupaza mosi na mvuke hewani.Hatahivyo, wataalamu wengi wa kisayansi wanatumai kwamba itaweezekana kuzuwia kupanda duniani kwa ujoto kwa kima cha digirii 2 Celicius.

Kwa nchi kama zile za visiwa mfano wa Madiven,Tuvalu au kisiwa cha Cook hilo ni joto kubwa tayari.Lakini ikiwa tutaweza kuzuwia kupandaa kwa ujoto kwa kima cha digrii 2,tutaweza kuepusha dhara kubwa .Lakini kufanikiwa hivyo,itawapasa wanadamu hadi ifikapo kati ya karne hii,kupunguza kwa nusu moshi wao unaopaa hewani.

Hiyo shabaha ya kupunguza mivuke na moshi kwa kiwango cha 5% chini ya makubaliano ya Kyoto,kwa kupunguzwa kwa hadi 50% kutachangia hatua ya mwanzo tu.Kwani nchi nyingi duniani ,hazitimizi hata shabaha iliowekwa na mapatano ya Kyoto.

Kwahivyo, nchini Spain,Ureno na Ireland uchafuzi wa mazingira na hali ya hewa kwa moshi unaopaa hewani kumeongezeka kwa kima cha kati ya 30 na 40%.

Ikiwa mapatano ya Kyoto yasituwame katika hatua yake ya kwanza,katka awamu yake ya pili kuanzia 2012,yatakabiliwa na changamoto tatu kubwa :

Kwanza,itapasa kuishawishi Marekani,mchafuzi mkubwa wa mazingira kujiunga na mapatano haya ya Kyoto.Kwani, wamarekani wanachafua robo-moja ya uchafuzi jumla duniani.Yule ambae kama rais George Bush anadharau kubadilika kwsa hali ya hewa katika sayari yetu,huyo hana dhamana.

Pili,dola zinazoinukia kama vile China ,india au Brazil nazo zijitwike nazo jukumu la kupunguza moshi wa viwandani.Ingawa moshi katika nchi hizo unaopaa juu ni mdogo kwa kila mkaazi kuliko ilivyo katika nchi za viwanda za kaskazini,lakini mwishoe,bila kushiriki kwa nchi za kusini mwa sayari hii,itakua viogumu kulinda kuchafuka zaidi kwa hali ya hewa.

Tatu na mwisho, misafara ya meli na ndege ambayo hadi sasa haikujumuishwa na makubaliano ya Kyto,ingebidi nayo kujumuishwa.Kwani uchafuzi wa moshi kutoka misafara ya ndege angani unatishia kuharibu kabisa shabaha ya kuunguza moshi huo kwa kima cha 5% iliowekwa na mapatano yaKyoto.

Serikali za dunia hii,zitakua zinafanya barab ara kutoka kupiga hatua ya pili katika njia ndefu ya kutunza hali ya hewa katika sayari hii.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW