MAPATANO YA SARAFU YA EURO MASHAKANI
22 Machi 2005Gazeti la TAGESSPIEGEL kutoka Berlin likiuchambua Umoja wa Mataifa laandika:
"UM lazima urekebishwe na juu ya swali hilo wengi wanakubaliana.Katibu mkuu Annan katika ripoti yake aliutumia wasaa wote alionao.Mapendekezo anayotoa ama kuhusu marekebisho ya Tume ya Haki za binadamu au mwito kwa mataifa tajiri kujitolea mwishoe kuchangia 0.7 ya pato lao la Taifa katika mfuko wa misaada ya maendeleo yanaingia akilini na yanastahiki."-ni maoni ya TAGESSPIEGEL mjini Berlin.
Ama gazeti linalotoka pia mjini Berlin-DIE WELT linachambua mapendekezo ya kurekebisha mapatano ya kuimarisha sarafu ya ulaya ya Euro.Laandika :
"Kanzela Schröder kueleza muafaka uliofikiwa kuwa ni ‘matokeo mema’ ni kashfa kwa Ulaya.....Na hasa Ujerumani na Ufaransa zimetumia sauti zao nzito katika Umoja wa sarafu bila kuona aibu kuyadhofisha hata zaidi makubaliano yanayoegemea sarafu ya Euro.Nchi hizo mbili hazikujishughulisha kuimarisha msingi wa Euro,bali inadhihirika kutoa sura nzuri alao karatasini baada ya mwaka au miaka 2 ijayo."-laandika DIE WELT.
SÜDDEUTSCHE ZEITUNG kutoka Munich linahisi kwamba, Ujerumani ilikua na jukumu barani Ulaya la kushika usukani wa kiuchumi.UU ukafuata fikra za Ujerumani za kudhibiti mashindano na baadae umoja wa sarafu wa Ulaya kama ilivyodai Ujerumani.......Uchumi wa Ujerumani unanufaika na muungano wa Ulaya –alao ndio msimamo wa Kanzela alietangulia Helmut Kohl.
Kanzela Scvhröder lakini,laandika gazeti- hana muelekeo.Anauhujumu UU mjini Brussels ikiwa kufanya hivyo kunampa nafuu ya kuvuta pumzi katika siasa za ndani.
Katika gazeti la kibiashara-HANDELSBLATT linalochapishwa Düsseldorf laandika kwamba, bila ya kizingiti cha 3%,mlango ungezidi kupanuka kwa wanasiasa kujitwika madeni zaidi.Masoko ya fedha kwahivyo yanadhani tena bila kukosea madeni yatazidi kuongezeka.Kupanda jana kwa riba za mikopo ya dola ni ushahidi wa hayo.
Gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINE kutoka Erfurt linataja upande mwengine wa swali hili:
Laandika:
"Sio mapatano ya kuimarisha sarafu ya Euro ndilo tatizo kwa Ujerumani,bali ukosefu wa uchumi wake kuweza
Hata gazeti la Bonn-GENERAL-ANZEIGER halikuvutiwa na uamuzi uliokatwa jana na mawaziri wa fedha wa UU.Laandika:
"Kutokana na maoni mengi na tofauti yaliotolewa juu ya uamuzi uliopitishwa –ni jambo moja tu ni muhimu:
Sarafu ya Euro imeshuka thamani kwa wiki 2 kuliko ilivyokua.Na hii inatokana na uamuzi uliopitishwa.Matamshi ya waziri wa zamani wa fedha Theo Waigel eti ‘3% ni 3% hauna maana tena.Kwani, Umoja wa Ulaya umevunja sehemu muhimu ya imani ya sarafu yake iliowekewa.
Tugeukie sasa gazeti la MÄRKISCHE ORDERZEITUNG kutoka Frankfurter Order.Laandika:
"Kitambo sasa ,mapatano ya Umoja wa sarafu ya Ulaya yakiuguzwa hadi kuaga kwake dunia.Lakini kuyazika sasa kabisa ,hakuna anaethubutu.Jina la anaeugua ni mapatano ya kuimarisha sarafu ya Euro.Ni mapatano yaliofikiwa kutokana na mbinyo wa Ujerumani mwishoni mwa 1996.
2005 imetumiwa kuungana tena kwa Ujerumani kama sababu ilioitwika mziogo mzito ujerumani na kubidi kuwa na madeni zaidi...."
Likitumalizia gazeti la BERLINER ZEITUNG laandika:
"Berlin na Paris zimeyaporomoa chini mapatano ambayo serikali ya Ujerumani kwa muda mrefu ikijivunia ni mafanikio ya wajerumani....
Muafaka uliofikiwa Brussels ndio mabaya kuliko wowote ambao ungeweza kufikiwa .Unabainisha kurejea katika mshikamano wa kitaifa na kuupa kisogo ule wa kimataifa."