Watu 55 wafa kwenye mapigano ya koo nchini Somalia
10 Juni 2024Haya ni kwa mujibu wa wakaazi na maafisa wa Afya katika taifa hilo la Pembe ya Afrika.
Kulingana na Farah Nur, mzee wa ukoo na mkaazi wa Herale, mgogoro kati ya koo za Dir na Marihan, uliibuuka siku ya Jumamosi huko Abudwaq na miji ya Herale wakizozania ardhi ya malisho na maeneo ya maji.
Wafanyakazi kutoka hospitali za Herale, Abudwaq na miji mengine wawili miji ya karibu wamelithibitishia shirika la habari la Reuters kuwa walihudumia 115 watu waliojeruhiwa katika mapigano hayo. Huku wakaazi wakiongeza kuwa watu waliofariki kutokana na ghasia hizo wakazikwa mara moja.
Ahmed Shire Falagle, mshauri wa usalama kwa mkuu wa eneo la Galmudug amesema wanaamini kuwa al Shabaab ilihusika moja kwa moja na tukio hilo alilolitaja kuwa la ajabu kwani koo hiyo zimekuwa zikishirikiana kama ndugu na kufanikiwa kulitokomeza kundi la al-Shabaab kutoka eneo la Galmudug.