MAPIGANO MAGHARIBI MWA SUDAN
24 Desemba 2003Matangazo
KHARTOUM: Waasi katika eneo la magharibi nchini Sudan wamesema wanamgambo wanaoiunga mkono serikali wamewaua watu 24 na kuwajeruhi wengine 25 katika kipindi cha siku nne za nyuma.Kwa mujibu wa msemaji wa kikundi cha waasi cha JEM magharibi mwa Sudan,ndege za kivita siku ya jumatatu,zilivishambulia vijiji viwili katika eneo hilo la Darfur.Lakini msemaji wa jeshi amepinga kuwa kulikuwepo mashambulio.Madai ya mashambulio hayo yametolewa wakati ambapo serikali ya Sudan na kikundi cha SPLA cha waasi wa kusini mwa Sudan,wanajaribu kukamilisha mkataba wa amani.Mazungumzo hayo ya amani yanasimamiwa na Kenya.
