1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKosovo

Mapigano kwenye nyumba ya watawa nchini Kosovo yamalizika

25 Septemba 2023

Watu waliojjifunika kwa vitambaa usoni waliwafyatua risasi polisi wa doria wa Kosovo, huku Pristina ikilaumu makundi ya uhalifu ya Serbia kwa uvamizi huo. Walivamia nyumba ya watawa karibu na mpaka wa Serbia.

Mmoja ya maafisa wa polisi wa Kosovo waliofika kwenye eneo la tukio la uvamizi wa nyumba ya watawa katika mji wa Banjska, Septemba 24,2023.
Mmoja ya maafisa wa polisi wa Kosovo waliofika kwenye eneo la tukio la uvamizi wa nyumba ya watawa katika mji wa Banjska, Septemba 24,2023.Picha: Str/AFP/Getty Images

Mapigano kati ya watu waliojihami kwa silaha na mamlaka za Kosovo katika nyumba ya watawa karibu na mpaka wa Serbia yamemalizika jana usiku, serikali ya Pristina imesema baada ya operesheni ya polisi ya kurejesha udhibiti kwenye eneo hilo.

Waziri wa mambo ya ndani wa Kosovo Xhelal Svecla amewaambia waandishi wa habari kwamba wamelidhibiti eneo hilo.

Tangazo hili linatolewa baada ya mapigano ya siku moja yaliyoanza baada ya polisi wa doria kuvamiwa karibu na kijiji cha Branjska mapema jana Jumapili na kusababisha kifo cha afisa wa polisi wa Kosovo na mwingine kujeruhiwa.

Waziri mkuu wa Kosovo Albin Kurti amesema wavamizi hao wapatao 30 hatimaye walizingirwa na polisi kwenye nyumba hiyo na kuwataka kujisalimisha.

Ametoa matamshi hayo masaa kadhaa baada ya kuliita tukio hilo kuwa ni ugaidi, huku akiitupia lawama serikari ya Serbia

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW