1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano makali yaendelea Bakhmut

12 Mei 2023

Mapigano makali yameripotiwa kwenye maeneo ya ndani na pembezoni mwa mji wa Bakhmut nchini Ukraine huku kukiwa na madai tofauti juu ya upande unaoshinda na ule unaoshindwa katika mapambano ya kuwania mji huo

Ukraine Bachmut Luftaufnahme Zerstörung
Picha: Libkos/AP Photo

Vikosi vya Urusi vimedai kupata mafanikio huko Bakhmut licha ya ukosoaji kutoka kwa mkuu wa kundi la mamluki wa kirusi la Wagner aliyesema "hali ni ngumu" kwenye uwanja wa mapambano. Msemaji wa wizara ya Ulinzi ya Urusi amekaririwa akisema vikosi vya nchi hiyo vinaendelea na hujuma zake mashariki mwa Bakhmut vikisaidiwa na kamandi ya jeshi la anga. Hata hivyo mwandishi habari wa vita wa televisheni ya taifa ya Urusi, amesema vikosi vya Urusi huenda vitakabiliwa na mzingiro kufutia mafanikio ya mashambulizi ya wanajeshi wa Ukraine kwenye maeneo kadhaa ya mji wa Bakhmut.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW