1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano makali yaendelea kushuhudiwa huko Uvira

8 Desemba 2025

Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa huko Uvira mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wanakabiliana na jeshi la Kongo linaloungwa mkono na wanajeshi wa Burundi

Mashariki mwa DRC I Wapiganaji wa kundi la M23 wanapambana na FARDC huko Uvira
Wapiganaji wa kundi la M23 huko Mashariki mwa DRC wanapambana vikali na jesho la Kongo FARDC likisaidiwa na wanajeshi wa BurundiPicha: Michel Lunanga/AFP/Getty Images

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kuwa raia wapatao 20 wakiwemo watoto wamejeruhiwa. Aidha, takriban wanajeshi 20 wa Burundi wameripotiwa kuuawa kwenye mapigano hayo tangu yalipozuka upya Jumatatu iliyopita. Hata hivyo, vyanzo kadhaa vya kijeshi vimeeleza kuwa kwa sasa  wanajeshi wa Burundi  wamewadhibiti waasi wa M23 na kuwasababishia pia hasara.

Pande zote mbili zinapigania udhibiti wa mji wa DRC wa Kamanyola ambao unapakana na mataifa ya Rwanda na Burundi na ambao kwa sasa unadhibitiwa na M23. Mapigano hayo yanaripotiwa ikiwa ni siku chache tu baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani kati ya rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi mjini Washington.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW