1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano makali yaendelea nchini Sudan

16 Mei 2023

Mapigano makali yameendelea katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum wakati jeshi la nchi hiyo likipambana vikali kwa lengo la kutaka kuvitimua vikosi vya RSF ambavyo wamekuwa wakikabiliana navyo kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Sudan Khartum | Kämpfe, Rauch
Picha: Ahmed Satti/Anadolu Agency/picture alliance

Mapigano hayo yamesababisha machafuko katika maeneo mengine ya nchi hiyo, hasa katika mji mkuu Khartoum na katika mkoa wa magharibi wa Darfur. 

Katika hatua za hivi karibuni, Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan ameamuru kufungwa akaunti zote za benki za kikosi pinzani cha kijeshi kinachoongozwa na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo. 

Milipuko yaendelea Sudan huku vita vikiingia mwezi wa pili

Hadi sasa takriban watu 200,000 wamelazimika kukimbilia nchi jirani huku wengine 700,000 wakiwa wakimbizi wa ndani. Vita hivyo vimezusha mgogoro mkubwa wa kibinaadamu ambao unatishia pia kuathiri eneo kubwa la ukanda huo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW