1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano makali yaendelea Ukanda wa Gaza

6 Desemba 2023

Jeshi la Israel linaripotiwa kufanikiwa kukizingira kabisa kitongoji cha Khan Younis baada ya operesheni kubwa ya ardhini eneo hilo, huku likidai kwamba wapiganaji wapatao 5,000 wa kundi la Hamas wameuawa.

Matokeo ya mashambulizi ya jeshi la Israel dhidi ya kitongoji cha Khan Yunis kwenye Ukanda wa Gaza.
Matokeo ya mashambulizi ya jeshi la Israel dhidi ya kitongoji cha Khan Yunis kwenye Ukanda wa Gaza.Picha: Ahmed Zakot/Reuters

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kwamba hali katika ardhi ya Palestina iliyozingirwa inazidi kuwa mbaya kadri muda unavyosonga mbele huku likisisitiza kuwa msaada unaowasili huko Gaza ni mdogo mno.

Soma zaidi: Israel yashambulia Khan Younis, kusini mwa Gaza

Maafisa wa jeshi la Israel walionukuliwa na mashirika ya habari ya AP na AFP wamesema makadirio yao ya idadi ya watu waliouawa Gaza ni sawa na yale yanayotolewa na Wizara ya Afya inayoongozwa na Hamas ambayo imesema kuwa hadi sasa watu 15,800 wameuawa. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW