1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano makali yazuka katika mpaka wa Uganda

8 Novemba 2021

Idadi kubwa ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaoendelea kuingia Uganda kufuatia mapigano yaliozuka hapo jana Jumapili imeleta mashaka kuhusu jinsi watakavyoshughulikiwa.

AMISOM - Soldaten in Somalia
Picha: picture alliance/AP Photo/Jones

Huku serikali ya Uganda ikithibitisha mapigano hayo kutokea kwenye maeneo ya mji wa Bunagana kwenye mpaka wa Kusini Magharibi, shirika la umoja mataifa UNHCR pamoja na lile la Msalaba mwekundu wanahofia kuwa hawataweza kuwahudumia mamia ya wakimbizi hao wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Mamia ya wakimbizi wanaongia Uganda wanaelezea kuwa wanayakimbia mapigano yaliyozuka nchi kwao. Kulingana na msemaji wa jeshi la Uganda hadi sasa haijathibitishwa mapigano hayo ni kati ya majeshi ya serikali na kundi gani la wapiganaji, licha ya uvumi kuwepo kwamba ni wapiganaji wa M23. soma HRW: M23 walitumika kupambana na waandamanaji DRC

Msemaji huyo Brigadier Flavia Bywekwaso amesema "Tumezungumza na watu walioko huko na wamethibitisha kuna mapigano kati ya majeshi ya DRC na kundi la wapiganaji lisilojulikana na hatuwezi kulitambua kwa sasa mapigano yalianza jana jioni na wakimbizi wamezifi kuingia kwa sababu yanaendelea."

soma Uganda yawakamata wapiganaji 40 wa M23

Meya wa mji wa Bunagana Ismail NDAYAMBAJE amethibitisha kuwa wamo katika mashaka makubwa ya kuwatunza wakimbizi hao walioingia Uganda ghafla kwa idadi kubwa bila kutarajiwa. Hofu na mashaka walio nayo watu wa sehemu hiyo ni jinsi watakatangamana na watu hao ambao yamikini hawajui lolote kuhusu hatari ya ugonjwa wa COVID 19.

Meya Ndayambaje ameiambia DW kwa njia ya simu kwamba wasiwasi ni mkubwa kwani hawa watu wa Congo hawana barakoa ya kuepusha COVID-19 na wengine wanaweza kuingia na bunduki.

soma Waasi wa M23 warejea Congo

Kwa upande wake shirika la umoja mataifa linalowashugulikia wakimbikizi UNHCR limelezea kuwa litalazimika kuitisha misaada zaidi kutoka kwa wahisani mbalimbali kwani hawana uwezo wa kuwahudumia wakimbizi ahao ambao hadi wakati wa kuandaa ripoti hii walikuwa wamezidi elfu tano wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Mwakilishi wa UNHCR Uganda Joel Boutroue amesema huenda tutahitaji kuwahamisha hadi kambi zingine ambayo ni operesheni kubwa kwa hiyo huenda tutatangaza hali ya hatari na kuomba ufadhili.

UNHCR inashirikiana na shirika la msalaba mwekundu kutoa huduma na misaada ya dharura kwa wakimbizi wanaowasili pamoja na kuiwasajili. Msemaji wa Shirika la Msalaba mwekundu Uganda Irene Nakasiita wanasema mapigano yanaendelea na kwa upande wetu tunajiandaa kutoa misaada ya kibinadam.

soma Uganda haiwataki waasi wa kundi la M23

Eneo kulikozuka mapigano hayo ni jirani kabisa na makutano ya mipaka ya Uganda, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikimaanisha kuwa baadhi ya wakimbizi wanaweza kuamua kukimbilia Rwanda. Ila hofu kwa upande wa Uganda ni uwekezano wa wapiganai kuingia ndani ya mipaka yake na ndipo majeshi yake yameanza kuweka doria na kuwachuja wakimbizi wanaoingia.

 

Lubega Emmanuel DW Kampala.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW