1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano mapya yazuka Mashariki mwa DRC

21 Oktoba 2024

Mapigano yamezuka kati ya waasi wa M23 na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wanajeshi wa Kongo wakiwa Kirumba Mashariki mwa DRC
Wanajeshi wa Kongo wakiwa Kirumba Mashariki mwa DRCPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Mapigano hayo mapya yalivunja makubaliano ya usitishwaji mapigano ambayo yalikuwa yamedumu kwa wiki kadhaa. Duru za eneo hilo zimeeleza kuwa alfajiri ya jana Jumapili, waasi wa M23 walipambana na wanamgambo wa Wazalendo na kuwajeruhi raia 14 wakiwemo vijana wawili.

Usitishaji mapigano kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda ulianza mapema mwezi Agosti kufuatia upatanishi wa Angola. Mazungumzo ya amani kati ya Kinshasa na Kigali yalikwama, lakini duru mpya ya mazungumzo imepangwa kufanyika mjini Luanda mwishoni mwa wiki ijayo.

Soma pia: Vita nchini Kongo imezua mzozo mbaya wa afya ya akili na msaada ni mdogo mno

Rwanda inadai kuwa kuwepo kwa kundi la Wahutu wenye msimamo mkali wa FDLR eneo hilo, ni tishio kwa usalama wake. Tangu M23 ilipoanzisha tena mashambulizi mwishoni mwa mwaka 2021, wameteka maeneo makubwa ya eneo hilo la mashariki mwa Kongo lenye  utajiri wa madini.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW