1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLibya

Mapigano Libya yasimama baada ya kuachiwa kwa kamanda Hamza

16 Agosti 2023

Mapigano makali kati ya makundi mawili hasimu nchini Libya yametulia baada ya kundi moja kumuachia huru kiongozi wa ngazi za juu wa upinzani waliyekuwa wakimshikilia.

Walinzi wa pwani wa Libya
Walinzi wa pwani wa LibyaPicha: Mahmud Turkia/AFP

Kushikiliwa kwa kiongozi huyo, kulichochoea mapigano hayo makali kabisa kushuhudiwa mwaka huu katika mji mkuu Tripoli.

Kamanda huyo Mahmoud Hamza alikamatwa na kikosi maalumu cha 444 akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mitiga, hatua iliyoibua mapigano kuanzia usiku wa Jumatatu kati ya makundi hayo makubwa kabisa.

Hata hivyo aliachiwa huru na kukabidhiwa kwa kundi la tatu ambalo halikuhusika kwenye mapigano hayo, duru za makundi hayo hasimu ziliarifu jana jioni.