SiasaSudan
Milipuko na milio ya risasi yaendelea kurindima Khartoum
20 Aprili 2023![Sudan Khartum | Flucht Bewohner vor Kämpfen](https://static.dw.com/image/65383205_800.webp)
Matangazo
Watu takribani 300 wameuawa tangu kuzuka kwa mapigano siku ya Jumamosi baina ya vikosi tiifu kwa mkuu wa majeshi Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake Mohamed Hamdan Daglo anayeongoza kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support forces RSF. Stephane Dujarric ni msemaji wa Umoja wa Mataifa.
Mapigano hayo yameingia siku ya sita leo baada ya makubaliano mengine ya kusitisha machafuko kuvunjika jana Jumatano. Kikosi cha RSF kilisema awali kwamba wanajeshi wake "wataheshimu kikamilifu usitishaji mapigano" kuanzia saa 12 jioni siku ya jumatano kwa muda wa saa 24 kama lillivyofanya jeshi. Lakini mashuhuda wamesema milio ya risasi iliendelea kusikika Khartoum usiku.