1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroNigeria

Mapigano ya kikabila yaua watu 20 Nigeria

20 Juni 2023

Watu wapatao 20 wameuliwa katika machafuko mapya ya umwagaji damu kati ya wafugaji na jamii za wakulima katika jimbo la Plateau katikati ya Nigeria.

Nigeria Jos City Plateua State
Picha: Kola Sulaimon/AFP/Getty Images

Watu wapatao 20 wameuliwa katika machafuko mapya ya umwagaji damu kati ya wafugaji na jamii za wakulima katika jimbo la Plateau katikati ya Nigeria.

Msemaji wa polisi katika jimbo hilo Alfred Alabo ameliambia shirika la habari la AFP Jumatatu jioni kwamba shambulizi hilo la hivi karibuni lililofanywa na wafugaji waliojihami na silaha lilizilenga jamii za wakulima siku ya Jumapili katika wilaya ya Barkin Ladi katika jimbo la Plateau.

Alabo amesema wamepokea taarifa kwamba watu wapatao 15 waliuliwa jana na watu wengine watano wamezikwa leo na hivyo kuifanya idadi ya watu waliouwawa kufikia 20. Jimbo la Plateau hushuhudia machafuko ya kikabila na mapigano ya visasi kati ya wafugaji waislamu wa jamii ya Fulani na jamii za wakristo hususan katika wilaya za Mangu, Barkin Ladi na Riyom.

Gavana wa jimbo la Plateau Caleb Manasseh Mutfwang  amelaani mauaji hayo na kutaka vikosi vya usalama kukomesha umwagaji damu na uchomaji wa mali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW