MigogoroAfrika
Mapigano ya makundi hasimu yaitikisa Tripoli
13 Mei 2025
Matangazo
Maafisa kadhaa wamearifu kuwa milio la risasi na milipuko ilisikika hadi mapema leo Asubuhi mjini Tripoli baada ya kuzuka jana usiku kufuatia kuuawa kwa kamanda mmoja mwenye nguvu anayeongoza kundi la wapiganaji wenye silaha.
Afisa mmoja wa serikali amesema Kamanda huyo Abdel-Ghani al-Kikli wa kundi la SSA aliuawa na kundi hasimu linalofahamika kwa jina la Brigedi 444.
Inaarifiwa makabiliano yalishuhudiwa zaidi kwenye kitongoji cha Abu Salim kusini mwa Tripoli. Wizara ya Afya imesema watu sita wameuawa na inafanya kazi kuzihamisha familia zilizokwama katikati ya mapigano.
Mapigano hayo yameilazimisha izara ya elimu kuzifunga shule zote leo Jumanne na masomo kwenye Chuo Kikuu cha Tripoli yamesimamishwa kwa muda usiojulikana.