1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yaendelea Kongo licha makubaliano ya amani

8 Desemba 2025

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, watu zaidi ya thelathini wamepoteza maisha katika mlipuko wa mabomu katika kijiji cha Sange ndani ya wilaya ya Uvira jimboni Kivu Kusini.

 Goma 2025 | Waasi wa M23
Waasi wa AFC/M23 mjini Goma Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Picha: Arlette Bashizi/REUTERS

Mashahidi wanasema mabomu hayo yalilipuliwa kufuatia hali ya kutoelewana kati ya askari wa Kongo waliokuwa na hasira baada ya mapambano makali ya mchana dhidi ya AFC/M23 katika maeneo ya Bwegera na Luberizi, Mashariki mwa Kongo.

Mashahidi wengine wanasema kuwa AFC/M23 waliingia katika vijiji vya Lubarika, Matale, Muhungu, Munanira, Luvungi siku ya Jumapili, ambavyo vilikuwa vimeachwa na wakazi waliokimbilia mji wa Uvira na vijiji vya pembezoni, chini ya mabomu yaliyokuwa yakilipuliwa na pande zote zinazopigana.

Mashahidi hao wanasema AFC/M23 walilenga pia vijiji vya Bwegera na Luberizi, hali iliyozua hofu katika vijiji vya Mutarule na Sange.

Hali ya kibinadamu Kivu Kusini inazidi kuzorota

Katika taarifa ya hivi karibuni, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu inaonya kwamba hali ya kibinadamu katika Kivu Kusini inazidi kuzorota kwa kasi kufuatia kushadidi kwa mapigano hayo makali ambayo yamesababisha majeruhi wengi na kusababisha idadi kubwa ya watu kuyahama makazi yao.

Nani ananufaika na machafuko ya Kongo?

03:05

This browser does not support the video element.

Kwa ushirikiano na shirika la Msalaba Mwekundu  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundi nasema ilifanikiwa kuwaondoa na kuwapeleka hospitalini mjini Uvira watu 21 waliojeruhiwa kwa risasi hadi mji wa Uvira.

Wakati Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix Tshisekedi akihutubia taifa leo, mkazi wa Bukavu Kashali Enama Erhahamwoba alimwomba ataje pia mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa

Jeshi la Kongo linakanusha kutekwa kwa maeneo kadhaa katika eneo la Uvira na AFC/M23 na kuonya dhidi ya uvumi unaoenezwa nawale linachowaita kuwa ni "maadui wa amani" kupitia mitandao ya kijamii.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW