1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yaendelea Rafah huku Biden akiilaumu Hamas

14 Juni 2024

Helikopta za Israel zimeshambulia mji wa Rafah, huku jeshi la ulinzi la Israel IDF, likiripoti mapigano katika maeneo ya kusini mwa Gaza.

Israel | vita vya Mashariki ya Kati
Vifaru vya kijeshi vya Israel vinaendelea kusonga mbele mjini RafahPicha: Mostafa Alkharouf/Anadolu/picture alliance

Hali ya wasiwasi pia inaendelea kuongezeka katika mpaka wa kaskazini kati ya Israel na Lebanon, huku kundi la Hezbollah ambalo ni mshirika wa Hamas likifanya mashambulizi zaidi kuyalenga maeneo ya kijeshi ya Israel. Raia mmoja wa Lebanon ameripotiwa kuuawa katika mashambulizi hayo. 

Rais wa Marekani Joe Biden amelilaumu kundi la Hamas kwa kuchelewesha kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa wiki sita, kuwachiwa mateka na ujenzi mpya wa Gaza. 

Blinken ataka suluhisho la kidiplomasia kati ya Israel na Lebanon

Hata hivyo afisa mkuu wa Hamas Osama Hamdan, amesema kundi hilo linataka usitishwaji wa kudumu wa mapigano na kuondolewa kabisa wanajeshi wa Israel kutoka Gaza lakini Israel inayapinga masharti hayo ya Hamas.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW