1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Daraja muhimu laharibiwa na mapigano Sudan

11 Novemba 2023

Daraja muhimu linalokatisha mto Nile kwenye mji mkuu wa Sudan, Khartoum limeharibiwa kwenye wimbi la hivi karibuni la mapigano kati ya jesi la taifa na wanamgambo wa kikosi kilichoasi cha RSF.

Khartoum, Sudan
Khartoum, SudanPicha: Wang Hao/Xinhua/IMAGO

Hayo yamethibishwa na pande hasimu zinazohusika na mzozo nchini humo katika taarifa zilizotolewa kwa nyakati tofauti leo Jumamosi.

Mashuhuda wameripoti kuwa kuna ishara za wazi za uharibifu wa daraja hilo la Shambat linaloziunganisha wilaya pacha za Khartoum Kaskazini na Omdurman kwenye mji mkuu wa taifa hilo.

Soma zaidi: Mapigano yaendelea kati ya jeshi la Sudan na RSF

Kulingana na picha zilizochapishwa mitandaoni ambazo hata hivyo shirika la habari la AFP limeshindwa kuzithibitisha zimeonesha karibu nusu ya daraja hilo limeharibiwa.  Magari yaliyoharibika pia yameonekana yakiwa kwenye kipande kilichosalia cha daraja hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW