SiasaSudan
Mapigano yaripotiwa kupungua mjini Khartoum, Sudan
30 Mei 2023Matangazo
Wakazi waliripoti mapigano Alasiri ya leo karibu na eneo la kambi ya jeshi iliyoko kusini mwa Khartoum. Lakini pia saa kadhaa kabla ya muda wa nyongeza ya usitishaji mapigano kutiwa saini walitoa taarifa ya mapigano makali katika miji mitatu ya Khartoum, Omdurman na Bahri.
Soma pia: Mkataba wa usitishaji mapigano Sudan warefushwa kwa siku tano zaidi
Vita hivyo vimesababisha karibu watu milioni 1.4 kukimbia makazi yao, wakiwemo zaidi ya 350,000 ambao wamevuka mpaka kuingia katika matiafa jirani.