SiasaUkraine
Mapigano yaongezeka mashariki mwa Ukraine
16 Julai 2023Matangazo
Kyiv ilifanya shambulio lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu ili kuchukua tena udhibiti katika eneo lililokaliwa na Urusi mwezi uliopita na limesonga mbele katika sehemu za mashariki na kusini.
Soma pia: Putin: Urusi ina hifadhi ya kutosha ya mabomu ya mtawanyiko kujibu mashambulizi
Kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram Naibu Waziri wa Ulinzi Hanna Maliar amesema kwamba vikosi vya Urusi vimekuwa vikishambulia kuelekea Kupyansk katika mkoa wa Kharkiv kwa siku mbili mfululizo.
Maliar amesema majeshi ya Urusi na Ukraine yalikuwa yakipigana karibu na jiji lililoharibiwa la Bakhmut lakini vikosi vya Ukraine vilikuwa vikisonga mbele taratibu katika upande wake wa kusini.