1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yapamba Moto Gaza.

Eric Kalume Ponda6 Januari 2009

Majeshi ya Israle yaliendeleza na mashambulizi yake dhidi ya Hamas katika miji kadhaa yenye idadi kubwa ya watu katika eneo la Gaza licha ya wito kutolewa kwa kusimamisha mapigano hayo.

Vifaru vya jeshi la Israel vikizingira maeneo ya miji katika ukanda wa Gaza.Picha: AP


Majeshi ya Israle yaliendeleza na mashambulizi yake dhidi ya Hamas katika miji kadhaa yenye idadi kubwa ya watu katika eneo la Gaza licha ya wito kutolewa kwa kusimamisha mapigano hayo.



Jeshi la Israel ambalo lilianza mashambulizi yake ya ardhini mwisho mwa wiki iliyiopita, yaripotiwa limezingira maeneo mengi yanayodaiwa yanatumiwa na wafuasi wa kundi la Hamas kufanya mashambulizi ya mizinga ya roketi dhidi ya Israel.

Hali ilivyo katika eneo hilo inatajwa kuwa ya kusikitisha huku hospitali zikifurika na wahanga wa mapigano hayo.


Kwa mujibu wa habari zinazotufikia hivi punde vifaru na ndege za kijeshi aina ya helkopta za Isarael zimefanya mashambulizi makali katika mji wa Khan Yunis ulioko kusini mwa eneo la Gaza,ambako pia yalikabiliana vikali na wafuasi wa kundi la Hamas ambao waliendelea kujibu mashambulizi hayo.


Mashambulizi hayo pia yamekuwa yakiendelea usiku kucha katika mji wa Gaza na miji miji mingine kama vile Beit Lahiya na Jabiliya ambako zaidi ya watu 20 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa akiwemo mtoto wa umri wa miezi sita.

Kadjalika jeshi la Israel limesema kuwa hadi sasa jumla ya wanajeshi wake wanne wameuliwa na wengine 79 kujeruhiwa tangu mashambulizi hayo yaanze.


Maafisa wa mashirika ya huduma za kibinadamu wametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati kuinusuru hali ilivyo katika eneo hilo la mashariki ya kati.


Maafisa wa huduma za matibabu katika eneo hilo la Gaza wanasema kuwa hali hiyo imezidi kuwa mbaya na hospitali nyingi za eneo la Gaza sasa zimekabiliwa na uhaba mkubwa wa madawa kutokana na idadi ya watu waliojeruhiwa wanaomininika katika Hospitali hizo.


Kadhalika maafisa wa mashirika ya misaada ya kibinadamu wanasema kuwa imekuwa vigumu kuwafikia mamia ya wakaazi wa Gaza wanaohitaji misaada kwa dharura kutokana na kwamba eneo hilo sasa limezingira na majeshi ya Israel


Shirika la masalaba mwekundi linasema kuwa magari ya ambulensi yameshindwa kufika katika eneo hilo la mapigano na huenda idadi ya watu waliofariki kutokana na mashambulizi ya usiku kucha ni kubwa zaidi kuliko ile iliyotolewa.


Mapigano hayo yaliyoanza tarehe 27 mwezi uliopita yamesababisha maandamano makubwa katika sehemu mbali mbali za ulimwengu huku Israel ikipuuza wito wa kusimamisha mapigano hayo. Israel inasema kuwa kamwe haitasimamisha mapigano hayo hadi pale itakapohakikisha kuwa uwezio wa kivita wa kundi la Hamas umevunjwa kabisa.


Wafuasi wa kundi la Hamas walianzisha mashambulizi ya mizinga ya roketi dhidi ya maeneo ya kusini mwaka Israel baada ya kukataa kuongeza muda wa m ktaba wa kusitisha mapigano uliomalizika tarehe 19 mwzi uliopita.

Mapigano hayo ambayo yametajwa kuwa makali zaidi kuwahi kutokea katika eneo hilo la mashariki ya kati.



Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW