1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yasababisha umwagaji damu kusini mwa Irak

19 Januari 2008

BAGHDAD: Si chini ya watu 70 wameuawa katika mapigano yaliyozuka nchini Irak kati ya wanajeshi na kundi la watu wa madhehebu ya Kishia.Polisi leo hii wamesema,hadi waumini 35 wa kundi fulani la kidini la Kishia,waliuawa katika mji wa Basra kusini mwa nchi na 18 wengine mjini Nasiriyah kama kilomita 350 kusini mwa mji mkuu Baghdad. Polisi na raia wa kawaida pia waliuawa katika mapambano hayo.