SiasaSomalia
Mapigano yaua watu 74 nchini Somalia
10 Februari 2023Matangazo
Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa msemaji wa mji unaokabiliwa na mapigano wa Las Anod.
Ghasia zilizuka katika mji huo siku ya Jumatatu, muda mfupi baada ya majimbo matatu katika eneo lililojitenga la Somaliland katika Pembe ya Afrika kutangaza kutaka kuwa sehemu ya Somalia tena.
Majimbo ya Sool, Sanaag na Cayn yanaunda takriban theluthi moja ya majimbo ya mamlaka ya Somaliland.Maeneo hayo yanazozaniwa pande zote mbili Somaliland na mamlaka ya jirani ya Puntland.
Vurugu katika ukanda huo zimedumu kwa majuma kadhaa sasa.