1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yazuka tena Kongo

23 Agosti 2013

Mapigano yanayoendelea baina ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika eneo la Kibati karibu na mji wa Goma, yanatajwa kuwa yamewaathiri raia katika eneo la mapigano.

Mapigano mashariki mwa Kongo
Mapigano mashariki mwa KongoPicha: Phil Moore/AFP/Getty Images

Mji wa Goma ulipigwa na mshtuko Alhamisi jioni, pale mabomu yalipokuwa yanavurumishwa katika mji huo. Ni kata za Katindo ya kushoto pamoja na Murara ndizo ziliathirika na mabomu hayo. Katika kata la Murara, duru toka machifu wa kata hizo zadokeza, kuwa watu watano ndio walijeruhiwa mukiwemo watoto watatu ambao hali yao ni mahututi.

Ili kuwakinga raia, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo, Martin Kobler, aliwaamuru wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kuhakikisha kuwa wanawalinda raia hao, huku msemaji wa Tume ya Umoja wa Mataifa katika Kongo hasa katika miji ya Beni na Butembo, Moussa Demba Dialo, akipewa muda wa masaa 44 kuondoka eneo hilo. Ilani hiyo imetolewa na mashirika ya kiraia.

Vita vya maneno vimezuka baina ya serikali za Rwanda na DRC. Rwanda kupitia msemaji wa jeshi lake Joseph Nzabamwita imesema kuwa Kongo kwa maksudi ilivurumisha roketi katika ardhi yake, jambo alilolitaja kuwa ni uchokozi mtupu.

Jeshi la UN kwenye tahadhari

Kwa upande wake msemaji wa serikali ya Kongo Lambert Mende Omalanga, ametangaza kuwa, mabomu yaliyoanguka Goma nakusababisha mahafa katika mji huo, yalitokea katika nchi jirani ya Rwanda. Navyo vita vikiwa bado vinaendelea baina ya jeshi la serikali ya DRC na waasi wa M23 katika kijiji cha Kibati, na ilikuwazuia waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma pamoja na kuwakinga raia, muwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa UN katika DRC Martin Kobler, aliamuru majeshi ya UN kufanya hima ilikuwakinga raia.

Wanajeshi wa Monusco wakilinda amani KongoPicha: Getty Images

Kauli hiyo inatokea, baada ya vituo vya Monusco pamoja na makaazi ya raia kulengwa na mashambulizi. Msemaji wa jeshi la UN katika DRC luteni kanali Félix Basse, akizungumza na redio ya UN Okapi alisema, kuwa tayari jeshi la UN liko kwenyi tahadhari, na kuwa liko tayari kukabiliana na waasi wa M23 ikiwa watasubutu kuusogelea mji wa Goma. "Kwa kweli tumezidisha mipango yetu ya ukingo na tumekuwa tukipiga doria katika viunga vya mji wa Goma na upande wa Sake, na huko Munigi tumeongeza idadi ya wanajeshi wetu, na Tuko tayari kukabiliana na waasi wa M23 ikiwa watasubutu kuelekea katika mji wa Goma," alisema Basse.

Wakati huo huo mashirika ya kiraia katika mji na wilaya ya Beni, yamempatia muda wa ma saa arubaini na nane, msemaji wa Monusco katika DRC hasa katika miji ya Beni na Butembo Bwana Moussa Demba Dialo. Mashirika ya kiraia katika mji na wilaya ya Beni, yamemupatia ma saa arubaini na nane kuondoka eneo hili. Na ikiwa hatatii amri ya mashirika ya kiraia, kwa madhara yatakayotokea atajijuwa mwenyewe.
Msemaji wa Monusco katika miji ya Beni na Butembo, anashukiwa na mashirika ya kiraia kuwatusi na kuita hatua yao yakutaka magari ya UN kutozunguka katika mitaa ya Beni kuwa ya utoto, na kuwa haikuathiri tume ya UN katika kazi zake.

Mwandishi: John Kanyunyu

Mhariri: Mohammed Khelef

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi