1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapinduzi ya Kenya: Nini kinafuata kwa kizazi cha Gen-Z?

13 Agosti 2024

Kizazi kipya cha wanaharakati kinaibuka katikati mwa jiji la Nairobi, kikiwa na simu za kisasa maarufu kama smartphone sambamaba na mtandao wa TikTok badala ya vipaza sauti na mabango.

maandamano-Kenya-Nairobi
Vijana walioshiriki maandamano ya KenyaPicha: Monicah Mwangi/REUTERS

Huku Kenya ikikabiliana na kupanda kwa gharama za maisha na sera za serikali zenye utata, Generation Z - neno linalotumiwa kwa ujumla kuelezea vijana waliozaliwa mwishoni mwa miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 - wameingia kwenye mkondo wa kidijitali, wakitumia nguvu ya mitandao ya kijamii kuchochea wimbi la maandamano na harakati za kisiasa dhidi ya utawala wa miaka miwili wa Rais wa Kenya William Ruto. Mahakama ya Kenya yaidhinisha kutuma jeshi huku vijana waandamanaji wakitafakari hatua inayofuata

Kile kilichoanza kama mikutano ya amani iliyoongozwa na vijana dhidi ya pendekezo la nyongeza ya ushuru ilichangia hatua pana zaidi dhidi ya Ruto na kile ambacho wengi wanaona kama matumizi mabaya ya serikali na ufisadi. Ruto, huku akisisitiza imani yake katika uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari, hadi sasa amekiri kishawishi cha kuzima mtandao lakini amechagua kutofanya hivyo, akidumisha usawa kati ya utawala na uhuru wa raia.

Maandamano ya KenyaPicha: Monicah Mwangi/REUTERS

TikTok, jukwaa la video fupi linalopendwa na Gen Z, limekuwa kitovu kisichowezekana cha mwamko wa kisiasa nchini Kenya. Video zake fupi, ambazo mara nyingi hujumuishwa na uchangamfu wa marejeleo, zimethibitishwa kuwa chombo chenye nguvu kwa vijana wa Kenya kueleza kutoridhika kwao, kushiriki uzoefu wao na kuungana na watu wenye nia moja. Waandamanaji vijana wa Kenya hawajaridhishwa na mawaziri wapya

Nikimnukuuu hapa mwandishi wa DW Edith Kimani  anasema "Video fupi ni mfalme. Wanatoa habari zinazoweza kumeng'enywa ambazo ni za uhakika na zinasogeza mbele majadiliano, unaburudika, lakini pia unafahamishwa kuhusu hali hiyo."

Mshikamano huu wa kidijitali haujachochea tu maandamano bali pia umekuza hisia ya jumuiya na madhumuni miongoni mwa wanaharakati wa Gen Z.

Jibu la serikali kwa vuguvugu hilo la kidijitali umekuwa mchanganyiko wa vitisho vilivyofichika na ushiriki wa tahadhari. Kukiri kwa Ruto kuhusu uwezo wa mitandao ya kijamii, pamoja na onyo kwamba anaweza kuzima mtandao, kumezua hali ya sintofahamu na hofu.

Waandamanaji Kenya ´wamkalia kooni´ Ruto

02:06

This browser does not support the video element.

Hofu ya kufuatiliwa na kulengwa imesababisha wanaharakati wengi kuchukua hatua mbalimbali za usalama, ikiwa ni pamoja na matumizi ya mitandao ya kibinafsi ya (VPN) ili kukwepa vikwazo vya mtandaoni, na mfumo wa mawasiliano wa siri. Wengine wamekataa kutaja majina yao halisi kwa waandishi wa habari kwa kuhofia kulipizwa kisasi.

Licha ya changamoto hizo, wanaharakati wa Gen Z wa Kenya hawajakata tamaa. Wanaendelea kutumia nguvu za mitandao ya kijamii kupaza sauti zao, kupinga hali iliyopo na kudai mustakabali mwema wa nchi yao. Matokeo ya vuguvuvugu hilo la kidijitali bado hayajulikani, lakini jambo moja liko wazi: mitandao ya kijamii imekuwa chombo muhimu kwa harakati za kisiasa nchini Kenya na kote barani Afrika. Waandamanaji warejea mitaani nchini Kenya kuipinga serikali

Huku serikali zikikabiliana na jinsi ya kukabiliana na ukweli huu mpya, Kimani alisema, wanaharakati vijana ambao wanaongoza vuguvugu hili wamedhamiria kuhakikisha kuwa sauti zao zinasikika, mtandaoni na nje ya mtandao.

Aliongeza kuwa sauti kizazi cha Gen Z cha Kenya na waandamanaji wengine zinasikika zaidi kuliko hapo awali, wakipinga hali iliyopo na kutetea mustakabali ambapo uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari sio tu maadili, lakini hali halisi.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW