Mapinduzi Zanzibar yatimiza miaka 48
12 Januari 2012![Viongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar pamoja na viongozi wa serikali ya muungano wa Tanzania katika sherehe za mapinduzi](https://static.dw.com/image/15661005_800.webp)
Matangazo
Leo Wazanzibari wameadhimisha miaka 48 ya mapinduzi ya Zanzibar yaliouondosha utawala wa kifalme.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika uwanja wa Amani/Unguja mjini ambako Rais wa Zanzibar, Dr. Ali Mohammed Shein, aliwahutubia wananchi. Katika maadhimisho hayo pia alihudhuria rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wa chama na serikali.
Mwandishi Othman Miraji
Mhariri Yusuf Saumu