1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maporomoko ya ardhi yawaua watu tisa Kivu ya Kusini

Saleh Mwanamilongo
24 Novemba 2024

Watu tisa wamekufa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia maporomoko ya ardhi huko Nyabibwe katika jimbo la Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Maporomoko ya ardhi yawaua watu tisa Kivu ya Kusini, Mashariki mwa Kongo
Maporomoko ya ardhi yawaua watu tisa Kivu ya Kusini, Mashariki mwa KongoPicha: GLODY MURHABAZI/AFP

Watu tisa wamekufa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia maporomoko ya ardhi huko Nyabibwe katika jimbo la Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Thomas Bakenga, mkuu wa mtaa wa Kalehe amesema nyumba kadhaa zilisombwa na mafuriko ya mvua na matope katika mji wa wakulima wa Nkubi na kuharibu mashamba kadhaa.

Waliofariki ni pamoja na Mama na watoto wake saba ambao nyumba yao ilifukiwa na tope. Na msichana mwengine alifariki katika kambi ya wakimbizi ya eneo hilo.

Kwa upande wake, Delphin Birimbi, mkuu wa asasi za kiraia katika mtaa wa Kalehe, amesema mvua hiyo ilisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu.

Mvua zinazoendelea kunyesha mara kwa mara husababisha mafuriko na vifo vya watu katika baadhi ya maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW