1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maporomoko na mafuriko yauwa watu 143 nchini Vietnam

11 Septemba 2024

Maporomoko ya ardhi na mafuriko yaliyoenea, yakisababishwa na kimbunga Yagi, yamesababisha vifo vya watu 143 nchini Vietnam. Kimbunga Yagi ndio kimbunga kibaya kabisa kuwahi kupiga kaskazini mwa Vietnam.

Athari za mafuriko huko Vietnam
Athari za mafuriko huko VietnamPicha: HUU HAO/AFP via Getty Images

Mapomoroko ya ardhi na mafuriko yaliyoenea, yakisababishwa na kimbunga Yagi, yamesababisha vifo vya watu 143 nchini Vietnam. Watu 58 bado hawajulikani waliko kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa leo Jumatano na mamlaka nchini humo. Juhudi za kutafuta waliotoweka pamoja na kutowa msaada zinaendelea. Kimbunga Yagi ndio kimbunga kibaya kabisa kuwahi kupiga kaskazini mwa Vietnam katika kipindi cha miaka 30, na kilipiga eneo zima hilo mnamo siku ya Jumamosi kikisababisha upepo mkali na mvua kubwa. Kimbunga hicho kilipiga pia Ufilipino na China ambako kilisababisha uharibifu mkubwa.