1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maporomoko ya ardhi yaua watu 10, DRC

10 Mei 2023

Watu kumi wamefariki katika maporomoko ya ardhi baada ya mvua kubwa kunyesha mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wakazi wa Nyamukubi wakitembea juu ya vifusi baada ya mafuriko makubwa katika mkoa wa Kalehe, Kivu Kusini mnamo Mei 6, 2023.
Mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamesababisha uharibifu mkubwa ikiwa ni pamoja na watu kupoteza maisha.Picha: GLODY MURHABAZI/AFP

Hayo yamethibitishwa leo na maafisa katika eneo ambalo mamia ya watu walifariki wiki iliyopita kufuatia mafuriko makubwa. Kiongozi wa eneo la Lubero, la mkoa wa Kivu Kaskazini Edgard Kasombolene amesema maporomoko hayo ya ardhi yalitokea jana usiku katika kijiji cha Miringati. Kamanda wa polisi wa Lubero Kanali Jean Habamungu amesema shughuli ya kuwatafuta walionusurika inaendelea. Mkasa huo wa karibuni unafuatia mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyoathiri mashariki mwa Kongo katika siku za karibuni. Zaidi ya watu 400 walikufa wiki iliyopita katika mkoa wa Kivu Kusini baada ya mafuriko makubwa kulikumba eneo la Kalehe la mkoa huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW