Maporomoko ya ardhi yauwa takriban watu 64 Ethiopia
12 Machi 2026
Matangazo
Manuqa, mkurugenzi wa idara ya kushughulikia majanga katika eneo hilo, amesema maporomoko hayo yalitokea katika eneo la Gamo na kuathiri wilaya ya Gacho Baba, Kamba na Bonke.
Manuqa amesema mtu mmoja alitolewa kwenye tope akiwa hai wakati wa shughuli ya uokoaji.
Mkuu wa mawasiliano wilayani Gacho Baba, Abebe Agena, amesema wengi wa waliokufa walipatikana wakiwa wamezikwa kwenye tope.
Idadi ya nyumba zilizoathirika bado haijabainika.
Rais wa jimbo la kusini mwa EthiopiaTilahun Kebede, ameelezea masikitiko yake juu ya maafa hayo na kuwataka wakazi kuhamia maeneo ya juu wakati mvua inaendelea kunyesha.