1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maporomoko ya ardhi yauwa watu 12 Kongo kufuatia mvua

15 Aprili 2024

Kiasi ya watu 12 wamekufa na zaidi ya 50 bado hawajulikani waliko baada ya mvua kubwa kusababisha korongo kuporomoka kwenye mto kusini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Maporomoko ya ardhi Kongo
Maporomoko ya Korongo yalisababisha udongo na vifusi kuanguka kwenye kingo za Mto Kasai na kuwafukia watuPicha: GLODY MURHABAZI/AFP

Kiasi ya watu 12 wamekufa na zaidi ya 50 bado hawajulikani waliko baada ya mvua kubwa kusababisha korongo kuporomoka kwenye mto kusini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Soma pia: Takriban watu 40 wamekufa kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo

Maporomoko hayo ya ardhi yalitokea Jumamosi saa sita mchana katika eneo la Dibaya Lubwe katika mkoa wa Kwilu. Tukio hilo lilisababisha udongo na vifusi kuanguka kwenye kingo za Mto Kasai, ambako boti ilikuwa inatia nanga na watu wakifua nguo.

Gavana wa mpito Felicien Kiway amesema miili 12 imeondolewa kwenye vifusi mpaka sasa, wakiwemo wanawake tisa, wanaume watatu na mtoto. Amesema matumaini ya kuwapata manusura ni madogo sana kwa sababu tukio hilo lilitokea saa 12 kabla na bado wanaendelea shughuli ya utafutaji kwenye udongo. Mratibu wa asasi ya kiraia ya eneo hilo Arsene Kasiama amesema maporomoko hayo ya ardhi pia yaliwaangukia watu waliokuwa wanafanya manunuzi sokoni.