1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMalaysia

Maporomoko ya ardhi yauwa watu 26 Malaysia

16 Desemba 2022

Watu wasiopungua 16 wamekufa leo na wengine 17 wamejeruhiwa baada ya kutokea maporomoko ya udongo kwenye eneo moja linalotumika kama kambi ya mapumziko nje kidogo ya mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpu

Malaysia | Erdrutsch in Batang Kali
Picha: Malaysia Civil Defence/AP/picture alliance

Watu wasiopungua 16 wamekufa leo na wengine 17 wamejeruhiwa baada ya kutokea maporomoko ya udongo kwenye eneo moja linalotumika kama kambi ya mapumziko nje kidogo ya mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur.

Inaaminika kulikuwa na watu wasiopungua 94 wakati mkasa huo ulipotekea na maafisa wa usalama wanashuku karibu watu wengine 20 huenda wamefukiwa na vifusi vya udongo.

Hadi kufikia sasa watu saba wamelazwa hospitali wakiwa na majeraha madogo na vikosi ya uokozi vikisaidiwa na mbwa wa polisi tayari vimetumwa kuwatafuta wengine wasiojulikana waliko.

Kambi hiyo ya mapumziko kwenye kitongoji cha Batang Kali ambayo huvutia makundi ya watu inapatikana jirani na eneo maarufu kwa shughuli za utalii la nyanda za juu za Genting

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW