1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maporomoko yasababisha vifo tena Kongo

4 Machi 2026

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, maporomoko mapya ya tope yamepiga chanzo cha sekta ya kimataifa ya coltan na kusababisha vifo vingi.

Mgodi wa madini ya Coltan huko Rubaya
Mgodi wa madini ya Coltan huko RubayaPicha: Jack Hill/News Licensing/IMAGO

Tarehe 3 Machi, wachimbaji wa madini kwa mifumo ya jadi walipoteza maisha yao katika machimbo ya Gasasa, kwenye eneo la migodi la Rubaya, mgodi mkubwa zaidi wa coltan nchini, ulioko takribani kilomita 70 kutoka mji wa Goma.

Eneo hilo liko chini ya udhibiti wa kundi la AFC/M23 tangu Aprili 2024.

Wakati eneo hili likiwa katikati ya mvutano wa kikanda na kimataifa kuhusu madini muhimu, uliochochewa pia na sera za rais wa Marekani Donald Trump kuhusu madini ya kimkakati, janga hili jipya linaweka wazi hali mbaya na hatarishi za kazi za wachimbaji wa jadi pamoja na shinikizo linaloongezeka katika eneo hili ambalo limekuwa muhimu kwa uchumi wa vita wa ndani.

Maporomoko Jumanne huko Rubaya

Jumatano asubuhi huko Rubaya, miili inaendeleakutolewa chini ya vifusi. Pikipiki zinashuka milimani zikiwa zimebeba maiti zilizofunikwa haraka haraka. Idadi kamili ya waliopoteza maisha bado haijajulikana, lakini mashahidi wanazungumzia mamia ya vifo.

Wachimba migodi wakifanya kazi katika mgodi wa Coltan huko RubayaPicha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Maporomoko hayo yalitokea mwishoni mwa siku, Jumanne tarehe 3 Machi, katika moja ya mashimo ya uchimbaji wa jadi kwenye eneo kubwa la Rubaya, linaloenea kwa makumi ya kilomita za mraba.

Uokoaji unafanywa na wachimbaji wenyewe. Wakiwa wameelemewa, wanaomba msaada:

"Tafadhali wasiliana na kiongozi wetu, baba Ushindi. Aite waokoaji na huduma za kiufundi. Tunahitaji msaada wa haraka. Hali ni mbaya sana. Watu wengi wamekufa. Kilichotokea Gasasa safari hii kinashangaza. Hakijawahi kutokea. Nimekiona kwa macho yangu, nawaambia, hali ni mbaya," alisema mchimbaji mmoja.

Huko Rubaya, maelfu ya wachimbaji wa jadi wanafanya kazi katika mazingira hatarishi sana.

Tangu kuchukuliwa kwa eneo hilo na AFC/M23, mgodi huu unazalisha mapato makubwa kupitia ushuru unaotozwa kwenye uzalishaji na biashara ya coltan, kulingana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Mji wa migodi, uliotekwa na kundi hilo la waasi Aprili 2024, unachangia sehemu kubwa ya usambazaji wa coltan duniani.

Lakini Rubaya pia imekabiliwa na ongezeko la msongamano wa watu.

Wakimbizi wa ndani kutoka maeneo kama Luke, Shugi na Katobo wanamiminika migodini kutafuta riziki. Kulingana na vyanzo vyetu, M23 Imepiga marufuku ujenzi wa kambi za wakimbizi na wamezuia baadhi ya shule kuwapokea. Matokeo yake ni familia kutengana, watoto kutenganishwa na wazazi wao, na watoto wengi waliokimbia makazi yao kushuka migodini kufanya kazi.

Ukosefu wa usalama Rubaya

Clovis Mafare, mwanachama wa asasi ya kiraia ya eneo hilo, anasema:

"Maporomoko haya hayajazuia wengine kuendelea kufanya kazi. Hapa wachimbaji wanaonekana kama panya: mmoja akianguka kwenye mtego, wengine wanaendelea. Wengi wanaokuja hawajui hatari za migodi hii. Wakazi wa Rubaya wenyewe huepuka migodi kwa sababu wanajua hatari yake. Ni lazima kupunguza idadi ya wachimbaji na kuheshimu kanuni za uchimbaji wa jadi.," alisema Clovis.

Waasi wa M23 wakiwa eneo la RubayaPicha: Camille Laffont/AFP

Katika eneo ya Rubaya ambalo limekuwa eneo hatarishi lisiloruhusiwa kufikiwa kwa mashirika mengi ya kibinadamu kutokana na ukosefu wa usalama, mashambulizi ya droni na maporomoko ya ardhi, juhudi za uokoaji ni chache.

Ikumbukwe maporomoko mengine katika mgodi wa Rubaya tarehe 28 Januari 2026 yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 300

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW