1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maputo. Msumbiji na Tanzania kujenga daraja.

16 Oktoba 2005

Rais Armando Guebuza wa Msumbiji jana Jumamosi ameanza ziara rasmi nchini Tanzania ambayo itakamilika kwa kuweka jiwe la msingi la daraja linalounganisha nchi hizo mbili.

Ujumbe wa Msumbiji , ukiwa ni pamoja na waziri wa mambo ya kigeni , waziri wa ujenzi na nyumba , ulikuwa unatarajiwa kukutana na rais anayeondoka madarakani nchini Tanzania Benjamin William Mkapa. Mradi wa ujenzi wa daraja la umoja ulikuwa na ndoto ya watu wawili walioongoza nchi zao kupata uhuru, marehemu Samora Machel wa Msumbiji pamoja na Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania . daraja hilo lilikuwa limepangwa kujengwa kwa muda wa zaidi ya miaka 30, lakini hakuna kilichofanyika kutokana na kukosa fedha za mradi huo.