MAPUTO. Ugonjwa wa Kifua Kikuu watishia bara la Afrika
26 Agosti 2005Matangazo
Mawaziri wa afya wa nchi za Afrika wamepitisha azimio kwamba ugonjwa wa Kifua kikuu ni janga linalo hitaji msimamo wa kisiasa ili kupambana na maambukizi yanayo enea kwa kasi barani Afrika.
Kamati maalum ya Shirika la afya duniani WHO kanda ya Afrika iliyo na wanachama 46 ambao ni mawaziri wa afya kutoka nchi za Afrika wamepitisha azimio hilo katika mkutano wao uliofanyika nchini Msumbiji.
Azimio hilo limeafikiwa baada ya takwimu za ugonjwa wa kifua kikuu kuongezeka mara tatu zaidi katika nchi 18 barani Afrika tangu mwaka 1990 na kuendelea kuua zaidi ya watu nusu milioni kila mwaka barani kote.