MAPUTO : Umoja wa Ulaya kuisadia Msumbiji euro milioni 2
25 Februari 2007Matangazo
Kamisheni ya Umoja wa Ulaya imetenga euro milioni mbili kuisadia Msumbiji baada ya nchi hiyo kupigwa na kimbunga kikali wakati ikiwa katika harakati za kujijenga upya baada ya mafuriko makubwa.
Watu watatu wameuwawa na sabini kujeruhiwa wakati kimbunga Favio kilipoipiga nchi hiyo hapo Alhamisi na kuangamiza mamia ya nyumba. Ndege ambayo tayari iko Congo italisaidia Shirika la Msalaba Mwekundu na Umoja wa Mataifa katika kusafirisha maji safi,nyumba za kujishikiza na madawa katika eneo lililoathirika.
Operesheni kubwa ya usafishaji inafanyika hivi sasa katika baadhi ya maeneo mashuhuri ya watalii yalioathirika nchini Msumbiji.