Maputo: Upinzani unaona hadaa katika uchaguzi wa Msumbiji
20 Novemba 2003Matangazo
Jana Msumbiji ilifanya chaguzi za miji, kama hatua ya kwanza ya kuondoka madarakani Rais Joaquim Chissano, ambaye atateremka kitini mwake mwakani baada ya kutawala karibu miongo miwili. Wengi miongoni mwa wapigaji kura milioni mbili , walitoa sauti zao katika miji 33, kwenye koloni hilo la zamani la Ureno, lakini chama cha upinzani Renamo kilikishutumu chama cha Chissano kwa kufanya udanganyifu. Miji yote 33 imekuwa ikitawaliwa na chama cha Frelimo, tangu Renamo na vikundi vidogo 15 kwa uchache viliposusia chaguzi zilizopita mwaka 1998.
