MAPUTO:Mke wa Bush ziarani Msumbiji
27 Juni 2007Matangazo
Mke wa Rais Bush wa Marekani, Laura Bush amewasili nchini Msumbiji hii leo katika ziara yake ya mataifa manne barani afrika.
Ziara hiyo ya Laura Bush ina nia ya kuangalia ni jinsi gani Marekani itasaidia vita dhidi ya Malaria na Ukimwi maradhi yanayouawa idadi kubwa ya watu barani humo.
Laura Bush amewasili akitokea Mali na Senegal, kabla ya kwenda Zambia.