1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marais Tshisekedi na Samia washuhudia uwekaji saini mikataba

24 Oktoba 2022

Rais Felix Tshisekedi amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania, huku mataifa hayo mawili yakikuabaliana kushirikiana katika masuala ya teknolojia pamoja biashara kwa kuboresha bandari za mipakani.

Marais Felix Tshisekedi wa DRC na Samia Suluhu Hassan wa Tanzania
Marais Felix Tshisekedi wa DRC na Samia Suluhu Hassan wa TanzaniaPicha: Tanzania State House

Eneo kubwa lililopewa umuhimu kwenye ziara hii ni kujenga miundombinu ya reli ya kisasa, na ujenzi huo utafanywa na mataifa hayo kupitia mkopo wa fedha kutoka Benki ya Dunia.

Mawaziri wa fedha wa Tanzania,Congo na Burundi hivi karibiuni walikutana Washington Marekani na maofisa wa Benki ya Dunia na pande zote ziliafikiana kuhusu mkopo huo ambao hata hivyo kiasi chake bado hakijajulikana.

Reli hiyo ya kisasa itajengwa kuanzia Kigoma, Tanzania na kupita nchini Burundi na hatimaye Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Mbali ya suala la uboreshaji wa miundombinu, Rais Samia Suluhu Hassan amesema yeye na mgeni wake wamezingatia pia eneo la ukuzaji biashara pamoja na teknolojia.

Usalama na biashara

 

Rais Tshisekedi asisitizia umuhimu wa amaniPicha: Tanzania State House

Suala la usalama limejitokeza pia kwenye ziara hii na viongozi hao wamesema kuna uhumu wa pande zote mbili kuendelea kuimarisha jambo hilo na kulinga na Rais Tshisekedi kunapokosekana amani la usalama fursa nyingine za maendeleo nazo zinatoweka.

Hatua ya viongozi hao kuahidi kuitupia macho sekta ya miundombinu hasa juhudi za kutaka kujenga reli ya kisasa imekaribishwa na wengi huku jamii ya wafanyabiashara ikiamani kuwa itasaidiia  kuondosha minyoroo ya kulega lega kwa biashara.

Pamoja na hayo sekta binafsi ya Tanzania inefunguliwa milango kwenda kuwekeza nchini DRC na tayari sekta hiyo inakusudia kwenda kujikita katika kilimo katika kile kinachotajwa kuwa hatua za kutaka kukabiliana na tishio la upungufu wa chakula linaloinyemelea dunia.

Rais Tshisekedi ambaye amezuru pia Zanzibaar ameondoka leo kurejea Kinshasa, akiagwa na mwenyeji wake, Rais Samia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW