1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marais wa Urusi na Ukraine kukutana Paris

9 Desemba 2019

Kabla mkutano wake na Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mkutano wa kilele wa unaolinganishwa na ule "uliofanyika Normandy" huko Paris Ufaransa, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky yuko kwenye shinikizo.

Kombobild Volodymyr Zelensky und Wladimir Putin

Anatafuta kuwa huru, ila iwapo ataafikiana makubaliano yoyote kuna hatari ya upinzani kutoka nyumbani kwake.

Matarajio ni makubwa, si katika vyombo vya habari wala katika ulingo wa siasa, msisimko ni sawa. Mkutano huo wa Jumatatu huko Paris uliopewa jina Mkutano wa Kilele wa kama ule wa Normandy huenda ukawa mwanzo wa mabadiliko. Kabla ya yote kumekuwa na uchambuzi wa mambo mengi kuhusiana na kukutana kwa wakuu wa nchi hizo za Ukraine, Urusi na Ujerumani na Ufaransa ambao ndio waandalizi wa mkutano huo. Wachambuzi wamekuwa wakiangazia ni yapi yanayoweza kuafikiwa na ni yapi yanayoweza kwenda mrama pia.

Rais Putin anaingia katika mkutano huo akitarajiwa kutoa ushindi

Upinzani nchini Ukraine unaounga mkono nchi za Magharibi umemuonya Rais Zelensky dhidi ya kuvuka mpaka atakapokutana kwa mara ya kwanza ana kwa ana na Putin. Shinikizo zaidi linatoka katika nchi za nje ambapo Rais wa Marekani Donald Trump pia amesema kuwa hii ni nafasi ya hatua kubwa mno kupigwa katika mzozo wa nchi hizo mbili.

Waandamanaji wa Ukraine wakitoa onyo kwa rais waoPicha: Reuters/V. Ogirenko

Rais Putin ataingia katika mkutano huo wa Normandy akitarajiwa kutoka na ushindi kutokana na utayari wa Zelensky wa kufanya lolote lile kwa ajili ya amani ya mashariki mwa Ukraine. Kuleta amani katika eneo hilo la nchi yake ndiyo iliyokuwa ahadi kuu ya mchekeshaji huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 41 baada ya kuchaguliwa kama rais.

Mikakati ya kupata amani katika eneo hilo iko katika makubaliano ya Minsk ya mwaka 2015 ambayo hayajatelekzwa. Urusi na Ukraine pamoja na eneo la mashariki linalotaka kujitenga na ambalo linaungwa mkono na Urusi wote wanarushiana lawama katika suala hilo.

Mkutano huu wa Normandy haujafanyika tangu mwaka 2016 kwa kuwa Urusi ilikuwa inamchukulia rais wa zamani wa Ukraine Petro Poroschenko kama kizuizi na ilikuwa haimtaki.

Putin ana wasiwasi kuhusiana na kuandaa uchaguzi maeneo yanayotaka kujitenga

Urusi inataka kuilazimisha Ukraine kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Waukraine wanaotaka kujitenga, kwa hiyo inavyoelekea ni kwamba Urusi inataka kujiwasilisha katika mkutano huo kama mpatanishi na wala sio sehemu ya mzozo.

Rais wa zamani wa Ukraine Petro PoroschenkoPicha: picture-alliance/ZUMAPRESS.com/S. Glovny

Wasiwasi mkubwa wa Putin lakini ni kuendelea kufanya uchaguzi katika maeneo ya Ukraine yanayotaka kujitenga kwani itakapofanya hivyo itakuwa imehalalisha kujitenga kwao.

Jambo jengine ambalo linaongeza wasiwasi katika mkutano huo wa Paris ni suala ambalo halijapata utatuzi la usafirishaji wa gesi kutoka Urusi kupitia Ukraine kuelekea Ulaya. Makubaliano yaliyoko kati ya Ukraine na Urusi yanakwisha Desemba 31 na majadiliano ya makubaliano yatakayofuata hayajazaa matunda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW