1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rubio kutafuta majibu ya shambulizi la Qatar na Netanyahu

15 Septemba 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amekutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, huku baadhi ya washirika wa Israel wakikasirishwa na hatua ya Israel kuishambulia Qatar.

Israel | Marco Rubio | Benjamin Netanyahu
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Marco Rubio Picha: Nathan Howard/AFP/Getty Images

Israel iliishambulia Qatar ikiwalenga viongozi wa Hamas. Hatua hiyo inahofiwa huenda ikaathiri juhudi za usitishwaji mapigano Gaza. 

Rubio amesema Marekani imekasirishwa na uamuzi wa Israel kuishambulia Qatar lakini sasa ni wakati wa kuangalia kipi kinafuata baada ya shambulizi hilo.

Rubio alipanga ziara ya Israel wiki moja kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa unaoongozwa na Ufaransa ulio na nia ya kuitambua Palestina kama dola huru hatua inayopingwa vikali na serikali ya Netanyahu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW