1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAREKA NA UFARASA UMOJA WA MATAIFA

6 Agosti 2006

NEW YORK/UMOJA WA MATAIFA:

Taarifa kutoka Um zinasema Marekani na Ufaransa zimefikia muafaka juu ya azimio la Baraza la Uslama lenye shabaha ya kusimamisha mapigano baina ya Israel na hizbollah kusini mwa Lebanon.Muafaka huo unasemekana kuitisha kusimamishwa haraka kwa mapigano ,lakini hauto wakati wa kufanya hivyo.

Wajumbe wa Ufaransa na uingereza wamearifu kwamba Baraza kamili la Usalama na wanachama wake 15 litakutana hivi punde kuyakagua mapatano hayo.Balozi wa M arekani katika UM John Bolton amesema anatarajia azimio kupitishwa mnamo siku 2 zijazo.Lebanon,imelikataa penedekezo hilo lililofikiwa na inadai kusimamishwa haraka kwa mapigano.Na Hizbollah inadai haitasimamisha vita hadi mwanajeshi wa mwisho wa Israel ameihama ardhi ya Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW