1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani “haitovumilia” vitendo vya Iran eneo la Hormuz

31 Januari 2026

Marekani imetoa onyo kwa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi cha Kiislamu cha Iran kwamba "haitovumilia vitendo visivyo salama” katika eneo la Ujia wa Bahari wa Hormuz, baada ya Tehran kutangaza mazoezi ya kijeshi ya majini.

Mgogoro kati ya Marekani na Iran | Boti ya mwendo kasi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC)
Mgogoro kati ya Marekani na Iran | Boti ya mwendo kasi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC)Picha: Morteza Nikoubazl/NurPhoto/picture alliance

Jeshi la Marekani limesema kuwa halitavumilia mienendo "isiyo salama” kama vile ndege kuruka juu ya meli za kivita za Marekani, au boti ndogo za kasi za Iran kukaribia meli za Marekani katika mazoezi hayo ambayo yamepangwa kufanyika kesho.Taarifa yake iliendelea kuonya kuwa Jeshi la Marekani lina kikosi chenye mafunzo ya hali ya juu na uwezo mkubwa zaidi duniani, na litaendelea kufanya kazi kwa viwango vya juu zaidi vya taaluma na kufuata kanuni za kimataifa na kuongeza kuwa IRGC ya Iran nayo inapaswa kufanya vivyo hivyo. Ujia wa Bahari wa Hormuz, njia ya maji yenye upana wa kilomita 55 kati ya Iranna Oman, ni moja ya njia muhimu zaidi duniani kwa usafirishaji wa mafuta kwenda nje ya nchi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW