1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Idadi ya visa vya watu kujiua yaongezeka

17 Agosti 2023

Takwimu mpya za vituo vya kudhibiti na kuzia magonjwa nchini Marekani vimechapisha data inayoashiria kwamba takriban watu 49,500 wamejitoa uhai mwaka jana.

Amoklauf in Texas
Picha: Stewart F. House/AFP/Getty Images

Idadi ambayo haijamuisha idadi ya mwaka huu lakini takwimu zilizopo zinaashiria kuwa visa vya kujitoa uhai vimeongezeka zaidi nchini humo kuliko wakati wowote tangu kuanza kwa Vita vya pili vya dunia.

Christina Wilbur mwanamke mwenye umri wa miaka 45 ambaye mwanawealijifyatulia risasi na kujiuamwaka jana, anasema kuna tatizo ukizingazia kadri idadi inavyoongezeka. Na kwamba juhudi zaidi zinahitajika katika kulitafutia suluhu tatizo hilo.

Wataalam wameonya kuwa kujiua ni ngumu, na kwamba hivi karibuni ongezeko linaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na viwango vya juu zaidi vya msongo wa mawazo na upatikanaji mdogo wa huduma ya afya ya akili.

Lakini changamoto kuu ni kuongezeka kwa upatikanaji wa bunduki, kwa mujibu wa Jill Harkavy-Friedman, makamu mkuu wa rais katika kituo cha utafiti cha Marekani Kuzuia Kujiua.

Soma pia:Watu kadhaa wauwawa kwa kupigwa risasi Texas, Marekani

Majaribio ya kujiua kwa bunduki huisha kwa vifo mara nyingi zaidi kuliko wale wanaotumia njia zingine, na mauzo ya bunduki yameongezeka na upatikanaji wake ukiongezeka zaidi nyumbani.

Waliojiua kwa bunduki waongozeka

Uchambuzi wa hivi majuzi wa Chuo Kikuu cha John Hopkins ulitumia data ya awali ya 2022 ili kuhesabu kwamba kiwango cha jumla cha watu waliojiua kwa bunduki nchini kilipanda mwisho mwaka hadi kiwango cha juu zaidi.

Waombolezaji wakiomboleza kifo cha mpendwa waoPicha: Joe Raedle/Getty Images

Watafiti waligundua kwamba kwa mara ya kwanza, kiwango cha kujiua kwa bunduki miongoni mwa vijana weusi (Wamerakani weusi) kilizidi kiwango kati ya vijana weupe.

Idadi ya watu wanaojiua nchini Marekani iliongezeka kwa kasi kutoka miaka ya 2000 hadi 2018, wakati kiwango cha kitaifa kikigonga kiwango chake cha juu zaidi tangu 1941. Mwaka huo rekodi ilikaribia vifo 48,300.

Mnamo mwaka 2019 kiwango kilipungua kidogo na kushuka tena mnamo 2020, mwaka wa kwanza wa janga la COVID-19, Wataalamu wengine wanafungamanisha takwimu hizona hatua za mwanzo za vita na majanga ya asili, wakati watu walipojumuika pamoja na kusaidiana.

Lakini mnamo 2021, watu waliojiua waliongezeka kwa asilimia 4 na mwaka jana, kulingana na data mpya, idadi iliongezeka kwa zaidi ya watu 1,000, na kufikia 49,449 ongezeko la asilimia 3.

Soma pia:Biden alaani shambulizi la shule huko Nashville

Vituo vya kudhibiti na kuzia magonjwa vimesema kwamba ongezeko kubwa zaidi lilionekana kwa watu wazima.

Vifo viliongezeka karibu 7% kwa watu wenye umri wa miaka 45 hadi 64, na zaidi ya 8% kwa wenye umri wa zaidi ya miaka 65 .

Kulingana na mganga mkuu wa vituo hivyo Dk. Debra Houry,watu wa makamo na wazee hupata matatizombalimbali kama kupoteza kazi au kupoteza mwenzi wao, na ni muhimu kupunguza unyanyapaa na vikwazovyengine kwao ili kupata msaada.

Kujiua kwa watu wazima wenye umri wa miaka 25 hadi 44 kuliongezeka kwa karibu asilimia1%. Data mpya inaonyesha kuwa kujiua imekuwa sababu ya pili ya vifo katika kundi hilo katika mwaka 2022, kutoka nambari 4 mwaka 2021.

Licha ya takwimu hizi za kutisha, wengine wanasema kuna sababu ya kuwa na matumaini. Huduma mpya ya simu ilizinduliwa kuripoti mgogoro mwaka mmoja uliopita, ikimaanisha mtu yeyote nchini Marekani anaweza kupiga 988 ili kufikia wataalam wa afya ya akili.

Raia wa marekani wanaongoza kwa kumiliki bunduki duniani

00:53

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW