1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani iko tayari kumruhusu Tsai Ing-Wen kuizuru nchi hiyo

9 Machi 2023

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, imeashiria inaweza kumruhusu kiongozi wa Taiwan Tsai Ing-Wen kuzuru California kukutana na spika wa bunge na kupuuza umuhimu wa hatua hiyo wakati kuna pingamizi kutoka China.

Taiwan Präsidentin Tsai hält ihre Neujahrsansprache
Picha: Taiwan Presidential Office/REUTERS

Spika wa bunge la Marekani Siku ya Jumanne, McCarthy alithibitisha kwamba atakutana na Tsai katika jimbo lake, na kujaribu kuepuka uwezekano wa kufanya ziara Taiwan, ambayo wabunge kisiwani humo, wanahofia huenda ikachochea jibu la kijeshi kutoka China.

WorldNews-Taiwan to be alert for China millitary sudden entry

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price,  alielezea safari inayotarajiwa ya Tsai kuwa ya kupita badala ya ziara nchini humo.

China imesema imefadhaishwa na taarifa za mkutano huo kati ya Tsai na McCarthy na inapinga vikali mawasiliano yoyote rasmi kati ya Marekani na Taiwan.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW