1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yashambulia maeneo ya waasi wa Kihouthi Yemen

Angela Mdungu
10 Novemba 2024

Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema ndege zake za kivita zimefanya mashambulizi ya anga Jumamosi usiku nchini Yemen katika maghala kadhaa ya silaha za kisasa za waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.

Mashambulizi ya Wahouthi Bahari ya Shamu
Moja ya meli zilizowahi kushambuliwa na waasi wa Kihouthi katika Bahari ya ShamuPicha: Houthi Military Media via REUTERS

Taarifa ya wizara hiyo inaeleza kuwa maeneo yaliyolengwa yalikuwa na silaha kadhaa zilizotumika kulenga meli za kijeshi na za raia zilizokuwa zikipita katika eneo linalotumiwa kimataifa kwenye bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden. 

Soma zaidi: Marekani yashambulia ngome 15 za Wahouthi, Yemen

Kwa upande wake Televisheni ya Wahouthi ya Al Masirah imethibitisha kuwa Marekani na Uingereza zilifanya mashambulizi matatu huko Al Sabeen Kusini mwa mji mkuu, Sanaa.  Nchi hizo zimekuwa zikiilenga miundombinu ya waasi hao  tangu Januari zikijibu mashambulizi yao dhidi ya meli zinazopita Bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden.

Soma zaidi: Waasi wa Houthi waapa kulipiza shambulizi la Israel kwenye bandari ya Hodeidah

Waasi wa Kihouthi wasema mashambulizi hayo yanalenga meli zenye uhusiano na Israel na yanaashiria kuonesha mshikamano na Wapalestina katika vita vinavyoendelea Gaza.